SEBULENI

Sunday, November 11, 2012

HATA SISI TUNAPENDA KANDANDA JAMANI



Wadada kutoka chuo cha sayansi ya jamii cha Royal college of Tanzania(RCT) Wakiwashangilia kaka zao wa Ngazi ya Astashahada na Stashada katika fani mbalimbali zitolewazo chuo hapo, Mpaka mwisho wa mpira Astashahada waliwafunga kaka zao wa Stashahada kwa goli tatu kwa bila,, chini ni mashabiki mchanganyiko wadada kwa wakaka Pamoja na Rais wao Mh Peter William wakicheki burudani

DAR KILA SEHEMU NI JALALA TU.

Hapa ni barabara ya Sam Nujoma iliyotengenezwa kwa Mabilion ya walipa kodi lakini watu wamegeuza ni eneo la kutupia takataka kila mahali katika barabara hiyo nzuri, je Tanroad mpo au Mnapulizwa tu na viyoyozi maofisin huku watu wakiharibu miundombinu muhimu kama barabara au jukumu hili ni la nani?

Monday, November 5, 2012

KENGE AKUTWA NDANI YA NYUMBA DAR




Kenge huyu alikutwa ndani ya nyumba jijini dar es salaam maeneo ya Ubungo kibangu akiwa kajificha chini ya jokofu au maarufu kama tulivyozoea 'friji' lakini wenye nyumba walibahatika kuumua na kuepusha madhara yoyote yale ambayo kenge huyo angeweza kuyaleta humo ndani haswa kwa watoto na wakina mama., JAMANI TUWENI MAKINI NA WANYAMA NA WADUDU WAKALI KAMA HAWA HASWA KWA AJILI YA USALAMA WA WATOTO WETU

HII NI HATARI SANA JAMANI KWA VIJANA HAWA!!


Hapa ni Ubungo darajani kuelekea mwenge ambapo kamera ya bwana peter mtaani iliwakuta Vijana hawa Wauzaji wa bidhaa ndogo ndogo au maarufu kama watu wawaitwavyo 'wamachinga' wakiwa wanafurahia maisha ili hali sehemu waliokaa ni hatari sana kwa maisha yao kama kwa bahati mbaya ikatokea tu gari moja kubwa kuacha njia na kuja hapo walipokaa, JE ITAKUWAJE? Vijana wenzangu acheni masiala jamani wengine mna familia na pia Taifa linawategemaea sana jamani.. chukueni tahadhari

MWENGE KWAKITHIRI KWA GEREJI BUBU




Eneo la mwenge jijini Dar es salaam limekithiri kwa 'gereji bubu' karibu kila kona ya eneo lote lile la mwenge stendi na viunga vyake na kuharibu muonekano wa eneo hilo na pia kuikosesha Serikali mapato kwani 'gereji bubu' hizi hazina anwani na ofisi za uhakika pia kutolipa kodi serikalini kwa mujibu wa sheria kutokana na uchunguzi uliofanya na mwandishi wetu bwana Peter william au peter mtaani wakati alipowahoji wahusika wa maeneo hayo ya mwenge

Friday, November 2, 2012

KAZI HAKUNA JAMANI HASWA KWA VIJANA

Vijana hawa niliwakuta mitaa ya Ubungo mataa wakiyavizia magari makubwa ya mafuta yanaporudi toka nje ya nchini au mikoani yalipopeleka mafuta japo nao wapate mabaki mbaki ya mafuta machafu nao wakayauze ili maisha yaendelee jamani, haya ndio maisha bora kwa Vijana?? Wabunge na Mawaziri Vijana wenzetu mpoo?? maisha haya mpaka lini jamani????

MZEE WA UPAKO AKEMEA 'UDINI' NCHINI



Mchungaji Maarufu wa kanisa la Maombezi la TUTASHINDA la Ubungo kibangu jijini dar es salaam Antony Lusekelo maarufu kama'Mzee wa Upako' amekemea Vikali suala la 'UDINI' ambalo limeibuka nchini mwetu kwa siku za hivi karibuni na kuhatarisha amani ya nchi yetu iliyodumu kwa miaka hamsini sasa na kuishauri Serikali kuwa Wakali na watu wanaotaka kuvuruga Amani yetu, Mzee wa Upako aliyasema hayo jumatatu ya wiki hii ofisini kwake kibangu alipokutana na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari kanisani kwake jijij dar. kwa habari kamili fuatilia vipindi vya 'TUTASHINDA' vinavyorushwa na Tv ya C2C Kila siku saa3 kamili usiku kwa Mahojiano kamili na waandishi hao