Sunday, November 11, 2012
HATA SISI TUNAPENDA KANDANDA JAMANI
Wadada kutoka chuo cha sayansi ya jamii cha Royal college of Tanzania(RCT) Wakiwashangilia kaka zao wa Ngazi ya Astashahada na Stashada katika fani mbalimbali zitolewazo chuo hapo, Mpaka mwisho wa mpira Astashahada waliwafunga kaka zao wa Stashahada kwa goli tatu kwa bila,, chini ni mashabiki mchanganyiko wadada kwa wakaka Pamoja na Rais wao Mh Peter William wakicheki burudani
DAR KILA SEHEMU NI JALALA TU.
Hapa ni barabara ya Sam Nujoma iliyotengenezwa kwa Mabilion ya walipa kodi lakini watu wamegeuza ni eneo la kutupia takataka kila mahali katika barabara hiyo nzuri, je Tanroad mpo au Mnapulizwa tu na viyoyozi maofisin huku watu wakiharibu miundombinu muhimu kama barabara au jukumu hili ni la nani?
Monday, November 5, 2012
KENGE AKUTWA NDANI YA NYUMBA DAR
Kenge huyu alikutwa ndani ya nyumba jijini dar es salaam maeneo ya Ubungo kibangu akiwa kajificha chini ya jokofu au maarufu kama tulivyozoea 'friji' lakini wenye nyumba walibahatika kuumua na kuepusha madhara yoyote yale ambayo kenge huyo angeweza kuyaleta humo ndani haswa kwa watoto na wakina mama., JAMANI TUWENI MAKINI NA WANYAMA NA WADUDU WAKALI KAMA HAWA HASWA KWA AJILI YA USALAMA WA WATOTO WETU
HII NI HATARI SANA JAMANI KWA VIJANA HAWA!!
Hapa ni Ubungo darajani kuelekea mwenge ambapo kamera ya bwana peter mtaani iliwakuta Vijana hawa Wauzaji wa bidhaa ndogo ndogo au maarufu kama watu wawaitwavyo 'wamachinga' wakiwa wanafurahia maisha ili hali sehemu waliokaa ni hatari sana kwa maisha yao kama kwa bahati mbaya ikatokea tu gari moja kubwa kuacha njia na kuja hapo walipokaa, JE ITAKUWAJE? Vijana wenzangu acheni masiala jamani wengine mna familia na pia Taifa linawategemaea sana jamani.. chukueni tahadhari
MWENGE KWAKITHIRI KWA GEREJI BUBU
Eneo la mwenge jijini Dar es salaam limekithiri kwa 'gereji bubu' karibu kila kona ya eneo lote lile la mwenge stendi na viunga vyake na kuharibu muonekano wa eneo hilo na pia kuikosesha Serikali mapato kwani 'gereji bubu' hizi hazina anwani na ofisi za uhakika pia kutolipa kodi serikalini kwa mujibu wa sheria kutokana na uchunguzi uliofanya na mwandishi wetu bwana Peter william au peter mtaani wakati alipowahoji wahusika wa maeneo hayo ya mwenge
Friday, November 2, 2012
KAZI HAKUNA JAMANI HASWA KWA VIJANA
Vijana hawa niliwakuta mitaa ya Ubungo mataa wakiyavizia magari makubwa ya mafuta yanaporudi toka nje ya nchini au mikoani yalipopeleka mafuta japo nao wapate mabaki mbaki ya mafuta machafu nao wakayauze ili maisha yaendelee jamani, haya ndio maisha bora kwa Vijana?? Wabunge na Mawaziri Vijana wenzetu mpoo?? maisha haya mpaka lini jamani????
MZEE WA UPAKO AKEMEA 'UDINI' NCHINI
Mchungaji Maarufu wa kanisa la Maombezi la TUTASHINDA la Ubungo kibangu jijini dar es salaam Antony Lusekelo maarufu kama'Mzee wa Upako' amekemea Vikali suala la 'UDINI' ambalo limeibuka nchini mwetu kwa siku za hivi karibuni na kuhatarisha amani ya nchi yetu iliyodumu kwa miaka hamsini sasa na kuishauri Serikali kuwa Wakali na watu wanaotaka kuvuruga Amani yetu, Mzee wa Upako aliyasema hayo jumatatu ya wiki hii ofisini kwake kibangu alipokutana na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari kanisani kwake jijij dar. kwa habari kamili fuatilia vipindi vya 'TUTASHINDA' vinavyorushwa na Tv ya C2C Kila siku saa3 kamili usiku kwa Mahojiano kamili na waandishi hao
''HII SIO OFISI YA CCM JAMANI''
Ukiiona Benderahii hapa juu inavyopepea kwa madaa unaweza ukasema ni nyumba ya mjumbe wa ccm wa shina au Ofisi ya ccm ya kata ya shina la mataa fulani, la hasha bali hapa kiukweli sio Ofisi hii jamani bali ni nyumba ya mtu ambae akili zake hazipo sawasawa ipo pale makutano ya barabara ya kwenda Muhimbili na jangwani na Azania sekondari anapoishi huyo bwana mkubwa kwa muda sasa, CCM MPOOOOO????
Saturday, October 27, 2012
DISKO TOTO BEI JERO (500)
Muhusika wa Ukumbi wa disko maeneo ya mwenge akichukuwa mia tano mia tano zake toka kwa watoto waliokwenda 'kuruka majoka' jana ukumbini hapo kwa kiingilio cha mia tano tu za kitanzania na kupata burudani mpaka mida ya saa mbili usiku.
MAJI SHIDA HADI SIKUKUU JAMANI, DUUU
Huku ndio makongo juu kwetu, Dawasco wamekatiwa Umeme na Tanesco kwa kutowalipa deni lao huku wakazi wengi wakiwa wamewalipa Dawasco madeni yao lakini Dawasco hawataki kuwalipa Tanesco na sijui ni kwanini jamani na kusababisha kero ya Ukosefu wa Maji kwa muda wa takribani miezi kadhaa sasa ni shida tu huku kwetu kwakweli jamani, wenzetu wakisherekea sikukuu ya idd sisi tunawaza tutaoga nini na kufuwaje nguo zetu, serikali maisha bora kwa Watanzania yapo wapi?? mbunge wetu mpendwa Mh. Halima Mdee, upo dada??
Thursday, October 25, 2012
HATUNA WA KUTUPELEKA SHULENI JAMANI
Watoto hawa waishio katika mazingira magumu ambapo maskani yao ni katikati ya jiji mitaa ya Posta ambao huishi maisha yao ya kila siku kwa kuomba omba na kuokota makopo na kuyauza ili kujikimu na Maitaji yao ya kila siku, 'Sisi ni yatima na hatuna wa kutupeleka shuleni japo tunapenda sana na sisi tusome ili baadae tuje kuishi maisha mazuri'' waliniambia watoto hao nilipowahoji asubuhi ya leo hii mitaa ya posta mpya... TUWASAIDIENI JAMANI TAIFA YA KESHO HILI!!!.........
UKAGUZI WA MAGARI
'POLISI JAMII' WAKISAIDIANA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI KIYAKAGUWA MAGARI HASWA YA ABIRIA KATIKA BAADHI YA MAMBO KATIKA MAGARI HAYO KAMA LESENI ZA USAFIRISHAJI WA ABIRIA(T.LA), ROAD LISENCE, TIKETI, BIMA, SARE, HUKU WOTE AMBAO WATAKAOKATISHA RUTI NA KUKUTWA NA MAKOSA MBALI MBALI HUTOZWA FAINI ZA SHILLINGI LAKI MOJA MPAKA LAKI MBILI NA NUSU KAMA NILIVYOAMBIWA NA NDUGU HUSSEN CHAMBELA AMBAE PIA NI KATIBU WA CHAMA CHA MADEREVA NA MAKONDA WA WILAYA YA ILALA HUKU AKIWA NA AFANDE FRANSIS ANDREW KAMA NILIVYOWAKUTA ASUBUHI YA LEO MITAA YA KATIKATI YA JIJI NA KUSEMA KUWA ZOEZI HILO NI LA MUDA MREFU.... 'SAFI SAANA'
'KITUO' KIMEDONDOKA JAMANI HAPA POSTA
Kituo hiki cha Posta mpya kikiwa kimedondoka chini kwa sababu ambazo hazikupatikana mara moja kama kilivyokutwa na bwana Peter Mtaani lakini wafanyabiashara ambao wapo pembeni walipoulizwa walisema kimedondoka takri bani mwezi mmoja sasa na kusababisha wahuni na watoto wa mtaani kulaa ndani yake nyakati za usiku na hata kunya humo humo ndani na kusababisha Kero kubwa katikati ya jiji ambapo kuna maofisi mengi na shughuli nyingi sana na kusababisha harufu kwa Abiria na Wafanyabiashara ndogo ndogo wa mitaa ya posta mpya,, JE manispaa ya Ilala Mpooo???
Tuesday, October 23, 2012
TUNAPITISHA 'GESI' HAPA JAMANI
MAFUNDI WA KAMPUNI YA UJENZI YA BQ WAKICHIMBA BOMBA LA KUPITISHA GESI BARABARA CHINI KWA CHINI ILI KUPITISHA BOMBA LA GESI KUTOKA KITUO CHA GESI UBUNGO NA KUISAMBAZA KATIKA MAENEO TOFAUTI TOFAUTI YA JIJI LA DAR ES SAALAM KATIKA ADHMA YA SERIKALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI NA WATU KUACHANA NA MATUMIZI YA MAFUTA NA MKAA AMBAYO KWASASA 'MKAA' KWANZA NI GHALI SANA NA YANAHARIBU MAZINGIRA KWA MOSHI NA KUKATWA SANA KWA MITI NA KUPUNGUZA VYANZO VYA MAJI NA KUIACHA NCHI YETU KATIKA JANGWA,,,. HEKO SERIKALI YETU.
DAMPO KATIKATI YA BARABARA JIJINI DSM
KWAKWELI MANISPAA YA KINONDONI 'INATIA HURUMA' SANA YAANI HAWANA HATA SEHEMU TENGWA NA MAALUMU YA KUKUSANYIA TAKATAKA KWA AJILI YA KWENDA KUZITUPA DAMPO KUU MPAKA WAKAGEUZA 'DAMPO' DOGO HAPA BARABARA YA SAM NUJOMA KARIBU NA MATAA YA MWENGE NA KUHARIBU MAANDAHARI NZURI YA BARABARA YA SAM NUJOMA NA BUSTANI AMBAYO WAO WENYEWE 'MANISPAA' HUTUMIA PESA NYINGI ZA WALIPA KODI KUILIMA NA KUTUNZA KILA SIKU, JAMANI KUWENI WABUNIFU MANISPAA YA KINONDINO MSIKAE TU MAOFISINI BALI TEMBEENI MITAANI MUONE HALI YA UCHAFU ILIVYOKUWA MBAAYA SAAAANA JAMANI
KAMARI MWENGE STANDI MCHANA KWEUPEE
VIJANA WAHA WALIOKATA TAMAA NA MAISHA NA KUJISUSA NA KUSAHAU NDOTO ZAO WALIZOKUWA WAKIOTA MIAKA KADHAA ILIOPITA KUWA WANGEKUJA KUWA ''WATU FULANI'' MUHIMU KATIKA NCHI YAO HII YA 'ASALI NA MAZIWA' YA TANZANIA LAKINI HAPA WAMEKATA TAMAA NA KUAMUA KUCHEZESHA MCHEZO WA KAMARI MAARUFU KAMA ''KARATA TATU'' AU WAWEZA SEMA KUWA ''ALIYEKULA KALA NA ALIYE LIWA KALIWA'' KAMA WALIVYOKUTWA PEMBENI YA STENDI YA MABARI YA NA MWANDISHI WETU BWANA 'PETER MTAANI' MITAA YA MWENGE NA BAADA YA KUJUWA KUWA WAMEPIGWA PICHA WALINIANBIA 'NIWALIPE PESA KWASABABU ETI KWAMBA NIMEWAPIGA PICHA NA KUNIPIGA MIKWARA MINGI AMBAYO HATA HIVYO HAIKUNITISHA CHOCHOTE NA HATA HAWAKUONESHA KUSTUKA KUWA WANAFANYA KOSA LA JINAI TENA MCHANA KWEEUPEEE, JAMANI WATANZANIA WENZANGU HUKU NI KUKATA TAMAA KWA VIJANA WETU KWA WELI,, JE WAHUSIKA MPOOOO, WABUNGE VIJANA MPOOOO? SERIKALI JE?
Monday, October 22, 2012
WILAYA YA KINONDONI NI CHAFU SAAAANA
Haya ni baadhi ya Maeneo ya wilaya ya kinondoni ambayo yamekithiri kwa UCHAFU kama yalivyokutwa na mwandishi wetu ambayo ni kigogo, mwenge, shekilango karibu na sokoni, urafiki, ubungo standi ya mabasi madogo ambapo kijana mmoja kwenye picha hapo chini alikutwa amekalia takataka nakugeuza matakataka kuwa 'sofa' lake, pia Uchafu umekithiri sana maeneo ya ubungo kibangu
Subscribe to:
Posts (Atom)