Saturday, October 27, 2012
DISKO TOTO BEI JERO (500)
Muhusika wa Ukumbi wa disko maeneo ya mwenge akichukuwa mia tano mia tano zake toka kwa watoto waliokwenda 'kuruka majoka' jana ukumbini hapo kwa kiingilio cha mia tano tu za kitanzania na kupata burudani mpaka mida ya saa mbili usiku.
MAJI SHIDA HADI SIKUKUU JAMANI, DUUU
Huku ndio makongo juu kwetu, Dawasco wamekatiwa Umeme na Tanesco kwa kutowalipa deni lao huku wakazi wengi wakiwa wamewalipa Dawasco madeni yao lakini Dawasco hawataki kuwalipa Tanesco na sijui ni kwanini jamani na kusababisha kero ya Ukosefu wa Maji kwa muda wa takribani miezi kadhaa sasa ni shida tu huku kwetu kwakweli jamani, wenzetu wakisherekea sikukuu ya idd sisi tunawaza tutaoga nini na kufuwaje nguo zetu, serikali maisha bora kwa Watanzania yapo wapi?? mbunge wetu mpendwa Mh. Halima Mdee, upo dada??
Thursday, October 25, 2012
HATUNA WA KUTUPELEKA SHULENI JAMANI
Watoto hawa waishio katika mazingira magumu ambapo maskani yao ni katikati ya jiji mitaa ya Posta ambao huishi maisha yao ya kila siku kwa kuomba omba na kuokota makopo na kuyauza ili kujikimu na Maitaji yao ya kila siku, 'Sisi ni yatima na hatuna wa kutupeleka shuleni japo tunapenda sana na sisi tusome ili baadae tuje kuishi maisha mazuri'' waliniambia watoto hao nilipowahoji asubuhi ya leo hii mitaa ya posta mpya... TUWASAIDIENI JAMANI TAIFA YA KESHO HILI!!!.........
UKAGUZI WA MAGARI
'POLISI JAMII' WAKISAIDIANA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI KIYAKAGUWA MAGARI HASWA YA ABIRIA KATIKA BAADHI YA MAMBO KATIKA MAGARI HAYO KAMA LESENI ZA USAFIRISHAJI WA ABIRIA(T.LA), ROAD LISENCE, TIKETI, BIMA, SARE, HUKU WOTE AMBAO WATAKAOKATISHA RUTI NA KUKUTWA NA MAKOSA MBALI MBALI HUTOZWA FAINI ZA SHILLINGI LAKI MOJA MPAKA LAKI MBILI NA NUSU KAMA NILIVYOAMBIWA NA NDUGU HUSSEN CHAMBELA AMBAE PIA NI KATIBU WA CHAMA CHA MADEREVA NA MAKONDA WA WILAYA YA ILALA HUKU AKIWA NA AFANDE FRANSIS ANDREW KAMA NILIVYOWAKUTA ASUBUHI YA LEO MITAA YA KATIKATI YA JIJI NA KUSEMA KUWA ZOEZI HILO NI LA MUDA MREFU.... 'SAFI SAANA'
'KITUO' KIMEDONDOKA JAMANI HAPA POSTA
Kituo hiki cha Posta mpya kikiwa kimedondoka chini kwa sababu ambazo hazikupatikana mara moja kama kilivyokutwa na bwana Peter Mtaani lakini wafanyabiashara ambao wapo pembeni walipoulizwa walisema kimedondoka takri bani mwezi mmoja sasa na kusababisha wahuni na watoto wa mtaani kulaa ndani yake nyakati za usiku na hata kunya humo humo ndani na kusababisha Kero kubwa katikati ya jiji ambapo kuna maofisi mengi na shughuli nyingi sana na kusababisha harufu kwa Abiria na Wafanyabiashara ndogo ndogo wa mitaa ya posta mpya,, JE manispaa ya Ilala Mpooo???
Tuesday, October 23, 2012
TUNAPITISHA 'GESI' HAPA JAMANI
MAFUNDI WA KAMPUNI YA UJENZI YA BQ WAKICHIMBA BOMBA LA KUPITISHA GESI BARABARA CHINI KWA CHINI ILI KUPITISHA BOMBA LA GESI KUTOKA KITUO CHA GESI UBUNGO NA KUISAMBAZA KATIKA MAENEO TOFAUTI TOFAUTI YA JIJI LA DAR ES SAALAM KATIKA ADHMA YA SERIKALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI NA WATU KUACHANA NA MATUMIZI YA MAFUTA NA MKAA AMBAYO KWASASA 'MKAA' KWANZA NI GHALI SANA NA YANAHARIBU MAZINGIRA KWA MOSHI NA KUKATWA SANA KWA MITI NA KUPUNGUZA VYANZO VYA MAJI NA KUIACHA NCHI YETU KATIKA JANGWA,,,. HEKO SERIKALI YETU.
DAMPO KATIKATI YA BARABARA JIJINI DSM
KWAKWELI MANISPAA YA KINONDONI 'INATIA HURUMA' SANA YAANI HAWANA HATA SEHEMU TENGWA NA MAALUMU YA KUKUSANYIA TAKATAKA KWA AJILI YA KWENDA KUZITUPA DAMPO KUU MPAKA WAKAGEUZA 'DAMPO' DOGO HAPA BARABARA YA SAM NUJOMA KARIBU NA MATAA YA MWENGE NA KUHARIBU MAANDAHARI NZURI YA BARABARA YA SAM NUJOMA NA BUSTANI AMBAYO WAO WENYEWE 'MANISPAA' HUTUMIA PESA NYINGI ZA WALIPA KODI KUILIMA NA KUTUNZA KILA SIKU, JAMANI KUWENI WABUNIFU MANISPAA YA KINONDINO MSIKAE TU MAOFISINI BALI TEMBEENI MITAANI MUONE HALI YA UCHAFU ILIVYOKUWA MBAAYA SAAAANA JAMANI
Subscribe to:
Posts (Atom)
