SEBULENI

Saturday, October 27, 2012

DISKO TOTO BEI JERO (500)


Muhusika wa Ukumbi wa disko maeneo ya mwenge akichukuwa mia tano mia tano zake toka kwa watoto waliokwenda 'kuruka majoka' jana ukumbini hapo kwa kiingilio cha mia tano tu za kitanzania na kupata burudani mpaka mida ya saa mbili usiku.

MAJI SHIDA HADI SIKUKUU JAMANI, DUUU



Huku ndio makongo juu kwetu, Dawasco wamekatiwa Umeme na Tanesco kwa kutowalipa deni lao huku wakazi wengi wakiwa wamewalipa Dawasco madeni yao lakini Dawasco hawataki kuwalipa Tanesco na sijui ni kwanini jamani na kusababisha kero ya Ukosefu wa Maji kwa muda wa takribani miezi kadhaa sasa ni shida tu huku kwetu kwakweli jamani, wenzetu wakisherekea sikukuu ya idd sisi tunawaza tutaoga nini na kufuwaje nguo zetu, serikali maisha bora kwa Watanzania yapo wapi?? mbunge wetu mpendwa Mh. Halima Mdee, upo dada??

Thursday, October 25, 2012

HATUNA WA KUTUPELEKA SHULENI JAMANI


Watoto hawa waishio katika mazingira magumu ambapo maskani yao ni katikati ya jiji mitaa ya Posta ambao huishi maisha yao ya kila siku kwa kuomba omba na kuokota makopo na kuyauza ili kujikimu na Maitaji yao ya kila siku, 'Sisi ni yatima na hatuna wa kutupeleka shuleni japo tunapenda sana na sisi tusome ili baadae tuje kuishi maisha mazuri'' waliniambia watoto hao nilipowahoji asubuhi ya leo hii mitaa ya posta mpya... TUWASAIDIENI JAMANI TAIFA YA KESHO HILI!!!.........

UKAGUZI WA MAGARI






'POLISI JAMII' WAKISAIDIANA NA ASKARI WA JESHI LA POLISI KIYAKAGUWA MAGARI HASWA YA ABIRIA KATIKA BAADHI YA MAMBO KATIKA MAGARI HAYO KAMA LESENI ZA USAFIRISHAJI WA ABIRIA(T.LA), ROAD LISENCE, TIKETI, BIMA, SARE, HUKU WOTE AMBAO WATAKAOKATISHA RUTI NA KUKUTWA NA MAKOSA MBALI MBALI HUTOZWA FAINI ZA SHILLINGI LAKI MOJA MPAKA LAKI MBILI NA NUSU KAMA NILIVYOAMBIWA NA NDUGU HUSSEN CHAMBELA AMBAE PIA NI KATIBU WA CHAMA CHA MADEREVA NA MAKONDA WA WILAYA YA ILALA HUKU AKIWA NA AFANDE FRANSIS ANDREW KAMA NILIVYOWAKUTA ASUBUHI YA LEO MITAA YA KATIKATI YA JIJI NA KUSEMA KUWA ZOEZI HILO NI LA MUDA MREFU.... 'SAFI SAANA'

'KITUO' KIMEDONDOKA JAMANI HAPA POSTA



Kituo hiki cha Posta mpya kikiwa kimedondoka chini kwa sababu ambazo hazikupatikana mara moja kama kilivyokutwa na bwana Peter Mtaani lakini wafanyabiashara ambao wapo pembeni walipoulizwa walisema kimedondoka takri bani mwezi mmoja sasa na kusababisha wahuni na watoto wa mtaani kulaa ndani yake nyakati za usiku na hata kunya humo humo ndani na kusababisha Kero kubwa katikati ya jiji ambapo kuna maofisi mengi na shughuli nyingi sana na kusababisha harufu kwa Abiria na Wafanyabiashara ndogo ndogo wa mitaa ya posta mpya,, JE manispaa ya Ilala Mpooo???

Tuesday, October 23, 2012

TUNAPITISHA 'GESI' HAPA JAMANI

MAFUNDI WA KAMPUNI YA UJENZI YA BQ WAKICHIMBA BOMBA LA KUPITISHA GESI BARABARA CHINI KWA CHINI ILI KUPITISHA BOMBA LA GESI KUTOKA KITUO CHA GESI UBUNGO NA KUISAMBAZA KATIKA MAENEO TOFAUTI TOFAUTI YA JIJI LA DAR ES SAALAM KATIKA ADHMA YA SERIKALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA GESI NA WATU KUACHANA NA MATUMIZI YA MAFUTA NA MKAA AMBAYO KWASASA 'MKAA' KWANZA NI GHALI SANA NA YANAHARIBU MAZINGIRA KWA MOSHI NA KUKATWA SANA KWA MITI NA KUPUNGUZA VYANZO VYA MAJI NA KUIACHA NCHI YETU KATIKA JANGWA,,,. HEKO SERIKALI YETU.

DAMPO KATIKATI YA BARABARA JIJINI DSM



KWAKWELI MANISPAA YA KINONDONI 'INATIA HURUMA' SANA YAANI HAWANA HATA SEHEMU TENGWA NA MAALUMU YA KUKUSANYIA TAKATAKA KWA AJILI YA KWENDA KUZITUPA DAMPO KUU MPAKA WAKAGEUZA 'DAMPO' DOGO HAPA BARABARA YA SAM NUJOMA KARIBU NA MATAA YA MWENGE NA KUHARIBU MAANDAHARI NZURI YA BARABARA YA SAM NUJOMA NA BUSTANI AMBAYO WAO WENYEWE 'MANISPAA' HUTUMIA PESA NYINGI ZA WALIPA KODI KUILIMA NA KUTUNZA KILA SIKU, JAMANI KUWENI WABUNIFU MANISPAA YA KINONDINO MSIKAE TU MAOFISINI BALI TEMBEENI MITAANI MUONE HALI YA UCHAFU ILIVYOKUWA MBAAYA SAAAANA JAMANI

KAMARI MWENGE STANDI MCHANA KWEUPEE


VIJANA WAHA WALIOKATA TAMAA NA MAISHA NA KUJISUSA NA KUSAHAU NDOTO ZAO WALIZOKUWA WAKIOTA MIAKA KADHAA ILIOPITA KUWA WANGEKUJA KUWA ''WATU FULANI'' MUHIMU KATIKA NCHI YAO HII YA 'ASALI NA MAZIWA' YA TANZANIA LAKINI HAPA WAMEKATA TAMAA NA KUAMUA KUCHEZESHA MCHEZO WA KAMARI MAARUFU KAMA ''KARATA TATU'' AU WAWEZA SEMA KUWA ''ALIYEKULA KALA NA ALIYE LIWA KALIWA'' KAMA WALIVYOKUTWA PEMBENI YA STENDI YA MABARI YA NA MWANDISHI WETU BWANA 'PETER MTAANI' MITAA YA MWENGE NA BAADA YA KUJUWA KUWA WAMEPIGWA PICHA WALINIANBIA 'NIWALIPE PESA KWASABABU ETI KWAMBA NIMEWAPIGA PICHA NA KUNIPIGA MIKWARA MINGI AMBAYO HATA HIVYO HAIKUNITISHA CHOCHOTE NA HATA HAWAKUONESHA KUSTUKA KUWA WANAFANYA KOSA LA JINAI TENA MCHANA KWEEUPEEE, JAMANI WATANZANIA WENZANGU HUKU NI KUKATA TAMAA KWA VIJANA WETU KWA WELI,, JE  WAHUSIKA MPOOOO, WABUNGE VIJANA MPOOOO? SERIKALI JE?

Monday, October 22, 2012

WILAYA YA KINONDONI NI CHAFU SAAAANA








Haya ni baadhi ya Maeneo ya wilaya ya kinondoni ambayo yamekithiri kwa UCHAFU kama yalivyokutwa na mwandishi wetu ambayo ni kigogo, mwenge, shekilango karibu na sokoni, urafiki, ubungo standi ya mabasi madogo ambapo kijana mmoja kwenye picha hapo chini alikutwa amekalia takataka nakugeuza matakataka kuwa 'sofa' lake, pia Uchafu umekithiri sana maeneo ya ubungo kibangu

KIBOKO YA KUNGURU HII HAPA



JE KUNGURU KWAKO NI TATIZO? WANAKUKOSESHA RAHA NA AMANI? WANAANUWA NGUO ZA WATOTO WAKO? JE WANAFUNUWA MPAKA SUFURIA KWA SISI WA USWAHILI TUNAOPIKIA NJE NA KUONDOKA NA VIPANDE VYA NYAM HATA KAMA INACHEMKAA? DAWA HII HAPA KAMA UNAITAKA WEWE NITAFUTE TU!!!!

Wednesday, October 17, 2012

FILAMU MPYA YA 'THE BIG BOSS' INAKUJA JIPANGE


WASANII MAARUFU WA SANAA YA FILAMU TANZANIA MBOTO NA CHIKI WAKIIGIZA KIPANDE "SCENE" MOJAWAPO KATIKA FILAMU MPYA NA KALI IENDAYO KWA JINA LA 'THE BIG BOSS' INAYOANDALIWA NA KAMPUNI YA SEKA BOY PRODUCTION CHINI YA BOSS WAKE NA  MTAYARISHAJI WAKE PIA 'THE BOSS' BWANA PAUL SEKA BOY NA KUPIGWA PICHA KITAALAMU NA KIUFUNDI NA SID WALEE WA C2C TELEVISION, JANA MAENEO YA KATIKATI YA JIJI.(PICHA NA PETER WILLIAM WA 'SEBULENI' WA C2C TV)

FULL BATA NDANI YA KIJIJI BEACH



















WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI CHA DAR ES SAALAM(D.S.J) WAKISHEREKEA SIKU YAO 'BASH' NDANI YA FUKWE NZURI NA SAFI YA KIJIJI BEACH ILIYOPO MAENENEO YA KIGAMBONI DSM MWISHONI MWA WIKI KATIKA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WAPYA CHUONI HAPO, HAFLA HIYO ILIYOFANA SANA ILIANDALIWA NA RAIS WAO MH. MAGRET AKISHIRIKIANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUNI HAPO PAMOJA NA WANAFUNZI WOTE KWA UJUMLA NA KUHUDHURIWA NA WAGENI MBALIMBALI KUTOKA TAASISI NA VYUO TOFAUTI IKIWA NI PAMOJA NA NDUGU ZAO WA KARIBU WA ROYAL COLLEGE OF TANZANIA WALIOWAKILISHA NA RAIS WAO MH. PETER WILLIAM HENRY